vitabu nivipendavyo

  • where have all the leaders gone,uongozi wetu na hatma ya Taifa letu,makuhadi wa soko huria

VIJANA TUAMKE

tunataka kuona vijana wasomi wanaoweza kuhoji mfumo wowote wa kisiasa na kiuchumi unaokandamiza jamii,siyo vijana akina 'ndiyo bwana'wanafiki,wenye nidhamu ya woga na wabeba vipeperushi vya mafisadi.kama vijana wasomi,tusipofanya hivyo,JAMII ITAOTA KUTU,ITASAGIKA NA KUTEKETEA

Monday, October 29, 2012

UHURU NI HAKI YA KUZALIWA NAYO

     Naweza kuwa mzee kimwili na kimaumbile ila roho yangu ni changa. Nataka niwe mchanga daima.Kila chema nitakacho kizungumza leo hii kitabaki kuwa kichanga daima.Kama mwili unazeeka ila roho hubaki changa,kwa njia hiyo hiyo ,wanaonekana kupunguza kasi ya harakati za uhuru wa kweli ila hamu,ambayo ni roho inaendelea kuishi na daima ipo.Hamuhiyo haiwezi pumzika mpaka tutakapo jikomboa.Uhuru ni haki yetu ya kuzaliwa nayo na inabidi tuwenayo.Kadiri roho hii inaishi ndani yangu,siwezi zeeka.kwani roho ni changa.Upepo hauwezi ipuliza mbali,silaha haziwezi kuivunja na hata moto hauwezi kuiangamiza.Kama tuliomba uhuru kwa wakoloni wa kiingereza na tukapata serikali yetu wenyewe inayojitawala,kamwe hatuwezi shindwa kawa na usawa wa aliye nacho na hasiye nacho nchini kwetu Tanzania.Mpaka hapa tunaonesha roho ya ukombozi tunayo na inaishi miongoni mwetu.Tunapaswa kufanya ni kuiamsha,na kuondoa janga la ujinga na akili ya ubinafsi.
    Kila mtu anatambua nini maana ya kujitawala maana yake nini?sisi sote si kila mtu angependa kujitawala na kuwa na uhuru wa kuona kweli maliasili,wanyama pori,madini na ardhi;wazawa tunafaidika pasipo kuona twiga na urefu wake wote ule anapakiwa na kusafirishw kwenda ng'ambo kihaini,hivi unaweza ukamruhusu mtu husiye mjua/mfahamu vyema aingie jikoni kwako ndani ya nyumba yako na kuanza kupika?najua si rahisi kuwa hivyo.Sote tuna haki ya msingi kujitawala vile inavyopaswa kuwa na kukubalika na wote na sio wanasiasa kuweka maisha ya watanzania mitaji yao na huku wao na familia zao huwa salama na tunaodhurika na machafuko ni sisi tulio wengi wananchi.Na kuwapa watoto wao nguvu ya kutawala na kutufundisha wananchi kuwa watawaliwa daima,mpaka mfumo unaokubalika zaidi hivi sasa ni wenye nguvu kiuchumi wengi ndio hupata fursa za kisiasa bila kupingwa na kuendelea kuamisha wanyama wetu kwenda nje na kufanya wananchi wengi walio masikini matumbo yetu kuingia ndani na kukutana na mgongo,na huku wao wakiwa wakubwa wa vitambi.
     Kama tunataka kubadilika na kuwa vyema,tunatakiwa tujitume na kupigania haki yetu ya uhuru wa kweli wa wananchi,na kwa hili tunahitaji watu pamoja na mifumo iliyo makini kweli kweli na wazi.Tunahitaji vijana wasomi wenye kuitumia elimu yao kumulika njia sahihi na kuweza kuhoji mfumo wowote unaokandamiza jamii na sio vijana akina ndiyo mzee vijana wapeperusha vipeperushi vya mafisadi.Tunahitaji kujitambua na vitendo kweli,vitakavyo sukumwa na watu wenye nidhamu,hatupaswi kutaja njia tu,ila vitendo katika njia.Nidhamu ni ufunguo wa mafanikio kwa wale viongozi walopata fursa ya kutuongoza katika maisha yetu.
Makundi na Maandamano yasiyopangika hayawezi leta lolote.Sote tunabidi tujitoe mmoja mmoja kiupekee kwa manufaa ya taifa kwa ujumla.Roho ya utaifa inabidi iokolewe,hili ndilo jukumu letu kubwa.Nchi hii ya Tanzania itafaidika endapo tu roho ya utaifa na uzalendo itaokolewa.Tanzania ni nchi ya walio elimika na wasioelimika,wenye kipato cha juu,kati na chini,wakulima na wafanya biashara,kila mtu anatakiwa awe na uhuru wa kweli nchini,masikini nae ana haki ya msingi kuwa kiongozi,kama anaweza kujiongoza kiakili katika maisha yake ya kila siku hato shindwa kuwa kiongozi mfano kuwa mbunge.Tunatakiwa kuamsha roho ya utaifa kwa masikini na matajiri wa nchi hii wote kwa usawa na sio ombi bali liwe jukumu letu sote.Masikini ana haki pia ya kuota ndoto ya kuwa mbunge,waziri na hata rais wa nchi hii na akiishi ndoto yake,namnukuu mwanasiasa mkongwe mweusi wa Marekani bwana Jesse Louis Jackson alisema "no one should negotiate their dreams.Dreams must be free to fly high.No government.no legislature,has a right to limit your dreams.You should never agree to surrender your dreams".Kwa tafsiri hisiyo sahihi tunaweza kusema hakuna anayeweza kupanga ndoto zao,ndoto inapaswa kuwa huru na inayorendeka ,hakuna dora,hakuna bunge,lenye mamlaka ya kuweka ukomo wa ndoto zako,hupaswi kukubari kuacha ndoto zako bure.
Wito huo wa roho ya utaifa imeshatolewa,sasa au milele,maadili ya tabia njema,kufikiria hasa katika ukweli na kuwajibika na mapambano ya katiba mpya ni vitu vinavyo hitajika kwa umakini mkubwa.Songa mbele huku ukimuamini MUNGU ,na malipo yake yatajazwa mwisho wa safari....

Mwandishi na; Michael Joseph Mwanjasi 

Monday, September 17, 2012

KIJANA KUWA TAJILI WA MAWAZO NA SIYO KUIGA MAISHA NA TAMADUNI

Itakua vigumu kumshawishi mtu aliyevaa sare za kijeshi kua ni raia.Kwa maana hiyo malaya atavaa nguo zinazofanana na shughuri yake,kwa mavazi mwanadam anajulisha marazi yake.Mtakatifu atajulikana kwa moyo wake na mavazi yake.Kwa maana hii usemi kua MUNGU huangalia roho tu umepotoshwa ili mwanadamu apatekunajisi mwili wake,maandiko yanaposema kuwa MUNGU huangalia roho yana maana kwamba kila jambo jema chanzo chake ni rohoni.
                              "MUNGU akaona kila kitu alichokifanya,natazama ni chema sana"
                                 Mwanzo 1;31
MUNGU akumuumba mwafrika peke yake akiwa mwema sana,bali watu wote kwa jinsi yao,kwa faidayao kutokana na mazingira alimwowaweka,na kwa ajili ya utukufu wake.Kwa maana hii mwafrika si mweusi kwa bahati mbaya . Kwa maana hii mzungu hawezi kuheshimika kwa kujipaka masizi ili awe mweusi na hivyo hivyo kujikwangua kujikwangua kwa mwafrika hakumfanyi kuwa mzungu.Kinyume chake,KUNAMDHALILISHA.Madhumuni ya msingi ya kuvaa ni kufunika mwili .Mavazi ya kukosesha ni machukizo kwa MUNGU.Hekima katika mavazi ni muhimu sana.Kama hutakua shahidi wangu siku hizi kuna wimbi la tabia za ajabu ajabu ktk jamii yetu
1/.Vipodozi na madawa ya kuchoma nywele vina madhara makubwa,ila tunavipenda
2/.Ulevi na utumiaji wa sigara kwa vijana wa kitanzania umeongezeka,mpaka wanawake nao days wanatupia sigara na ni walevi
3/.Mavazi ya vishawishi kwa dada zetu yamekubalika tayari wanavaa nguo wanaachia kifua kionekane,mapaja kuonekana na yenye kubana na kuonesha ramani ya mwili wako wote.
4/.Kusahau hali za maisha na tuliko toka kwa vijana wa vyuoni tanzania imekua fasheni mtu anasahau kua familia yake imeuza shamba ili yeye asome lakini watu tunajisahau.
MWISHO namnukuu dada yangu Riyama Ally aliniandikia hivi siku moja "Naamini kuwa ukijitambua utaweza kumtambua muumba wako,utaweza kutambua majukumu yako wazazi wako dini yako kwa kufanya ibada na kuwatambua wanaokuzunguka kwa namna ya kuwaheshimu na kujiheshimu.Duniani kote hakuna star zaidi ya MUNGU.Ni mapito tu ambayo kesho hayata kuwa na nafasi mbele za MUNGU.Amal yako njema na ibada ndizo zitakazo kuweka katika pepo na kukuingiza katika ufalme wa MUNGU "
VIJANA TUACHE KUIGA NA KUISHI MAISHA TOFAUTI NA ASILI ZETU.

Monday, September 10, 2012

KICHWA KINA MENGI KIJANA MWENZANGU

Kichwa chako kina ubongo ambao hufanya kazi ya kutoa na kupokea mawimbi ya mawazo yanayotolewa na ubongo wa watu wengine.Ni sehemu pekee ambayo binadamu hupokea na kutunza mawazo au fikra za aina fulani.Maajabu makubwa na ugunduzi ambao binadamu hufanya huanzia katika fikra alizonazo,vilevile utajiri wa binadamu huanzia katika mitazamo yake ya kutumia fikra alizo nazo juu ya maisha yake na mazingira yake yanayomzunguka kwa wakati fulani.Maisha ya binadamu huongozwa na nguvu ya fikra zitokanazo kichwani mwake kwa mfumo wa imani aliyonayo ya maisha yake hapa duniani.MWISHO Kila mwanadamu wa dunia hii anakitu ndani yake kinachoweza kutubadili sisi jinsi tunavyoishi,tunavyocheza na tunavyotenda...............KIJANA TUMIA FIKRA ZAKO KATIKA KUBADILISHA MAISHA YAKO NA JAMII INAYOKUZUNGUA KWA KUWAZA FIKRA SAHIHI KWA MALENGO SAHIHI KWAKO NA JAMII

Thursday, September 1, 2011

Wasomi wanakuwapo kwa ajili ya jamii na siyo kinyume chake.Wajibu mkubwa wa msomi ktk jamii ni kukidhi mahitaji ya jamii yake ambayo inaundwa pia na wasio na elimu.Msomi anapaswa kumulika njia,ni mshika kurunzi.Tatizo la mtazamo huu ni jinsi msomi huyu anavyoshirikishwa ktk kubainisha mahitaji ya jamii yake.Swali la kujiulza hapa ni je?nani anayepanga mahitaji ya jamii,ni watu?ni viongozi?viongoz wa aina gani?je ni sahihi kwa jamii kwamba wenye nguvu ya pesa ndio washike hatamu za uchumi wa nchi,utawala na siasa?WAPI ELIMU KWA MTANZANIA?MH!bado taratibu tutafika

Wednesday, August 24, 2011

kuna usemi usemao ''mtoto ni taifa la kesho''siupingi kwani umekuwa imara tokea enzi za baba wa taifa hayati Mwl.Nyerere,usemi huo ulikuwa ukionekana upo hai,lakipi kwa sasa kuna usemi ''mtoto ni taifa la leo na kesho''nao siupingi kwani umelenga kuwa ndio nguvu ya Taifa sasa cha muhimu ni jinsi gani mtoto huyu anavyo wezeshwa kufikia kuwa taa ya Taifa kwa kumpatia malezi bora na ELIMU BORA,kwa sasa hakuna ubishi wanafunzi tumekumbwa na matokeo hatari kwa maendeleo ya nchi yetu na kiwango cha elimu kimeshuka,sasa tunamrithisha nini mtoto huyu hasa mtoto wa mkulima na masikini ambaye elimu ndio urithi wake pekee,kwani wenye nazo wako salama na familia zao na pesa ya kununua mtihani ipo,SASA WAPI MTOTO MWENZANGU WA MKULIMA NA MASIKINI WA MTANZANIA,AMKA TUPAMBANE KUPATA ELIMU BORA.