vitabu nivipendavyo

  • where have all the leaders gone,uongozi wetu na hatma ya Taifa letu,makuhadi wa soko huria

VIJANA TUAMKE

tunataka kuona vijana wasomi wanaoweza kuhoji mfumo wowote wa kisiasa na kiuchumi unaokandamiza jamii,siyo vijana akina 'ndiyo bwana'wanafiki,wenye nidhamu ya woga na wabeba vipeperushi vya mafisadi.kama vijana wasomi,tusipofanya hivyo,JAMII ITAOTA KUTU,ITASAGIKA NA KUTEKETEA

Monday, October 29, 2012

UHURU NI HAKI YA KUZALIWA NAYO

     Naweza kuwa mzee kimwili na kimaumbile ila roho yangu ni changa. Nataka niwe mchanga daima.Kila chema nitakacho kizungumza leo hii kitabaki kuwa kichanga daima.Kama mwili unazeeka ila roho hubaki changa,kwa njia hiyo hiyo ,wanaonekana kupunguza kasi ya harakati za uhuru wa kweli ila hamu,ambayo ni roho inaendelea kuishi na daima ipo.Hamuhiyo haiwezi pumzika mpaka tutakapo jikomboa.Uhuru ni haki yetu ya kuzaliwa nayo na inabidi tuwenayo.Kadiri roho hii inaishi ndani yangu,siwezi zeeka.kwani roho ni changa.Upepo hauwezi ipuliza mbali,silaha haziwezi kuivunja na hata moto hauwezi kuiangamiza.Kama tuliomba uhuru kwa wakoloni wa kiingereza na tukapata serikali yetu wenyewe inayojitawala,kamwe hatuwezi shindwa kawa na usawa wa aliye nacho na hasiye nacho nchini kwetu Tanzania.Mpaka hapa tunaonesha roho ya ukombozi tunayo na inaishi miongoni mwetu.Tunapaswa kufanya ni kuiamsha,na kuondoa janga la ujinga na akili ya ubinafsi.
    Kila mtu anatambua nini maana ya kujitawala maana yake nini?sisi sote si kila mtu angependa kujitawala na kuwa na uhuru wa kuona kweli maliasili,wanyama pori,madini na ardhi;wazawa tunafaidika pasipo kuona twiga na urefu wake wote ule anapakiwa na kusafirishw kwenda ng'ambo kihaini,hivi unaweza ukamruhusu mtu husiye mjua/mfahamu vyema aingie jikoni kwako ndani ya nyumba yako na kuanza kupika?najua si rahisi kuwa hivyo.Sote tuna haki ya msingi kujitawala vile inavyopaswa kuwa na kukubalika na wote na sio wanasiasa kuweka maisha ya watanzania mitaji yao na huku wao na familia zao huwa salama na tunaodhurika na machafuko ni sisi tulio wengi wananchi.Na kuwapa watoto wao nguvu ya kutawala na kutufundisha wananchi kuwa watawaliwa daima,mpaka mfumo unaokubalika zaidi hivi sasa ni wenye nguvu kiuchumi wengi ndio hupata fursa za kisiasa bila kupingwa na kuendelea kuamisha wanyama wetu kwenda nje na kufanya wananchi wengi walio masikini matumbo yetu kuingia ndani na kukutana na mgongo,na huku wao wakiwa wakubwa wa vitambi.
     Kama tunataka kubadilika na kuwa vyema,tunatakiwa tujitume na kupigania haki yetu ya uhuru wa kweli wa wananchi,na kwa hili tunahitaji watu pamoja na mifumo iliyo makini kweli kweli na wazi.Tunahitaji vijana wasomi wenye kuitumia elimu yao kumulika njia sahihi na kuweza kuhoji mfumo wowote unaokandamiza jamii na sio vijana akina ndiyo mzee vijana wapeperusha vipeperushi vya mafisadi.Tunahitaji kujitambua na vitendo kweli,vitakavyo sukumwa na watu wenye nidhamu,hatupaswi kutaja njia tu,ila vitendo katika njia.Nidhamu ni ufunguo wa mafanikio kwa wale viongozi walopata fursa ya kutuongoza katika maisha yetu.
Makundi na Maandamano yasiyopangika hayawezi leta lolote.Sote tunabidi tujitoe mmoja mmoja kiupekee kwa manufaa ya taifa kwa ujumla.Roho ya utaifa inabidi iokolewe,hili ndilo jukumu letu kubwa.Nchi hii ya Tanzania itafaidika endapo tu roho ya utaifa na uzalendo itaokolewa.Tanzania ni nchi ya walio elimika na wasioelimika,wenye kipato cha juu,kati na chini,wakulima na wafanya biashara,kila mtu anatakiwa awe na uhuru wa kweli nchini,masikini nae ana haki ya msingi kuwa kiongozi,kama anaweza kujiongoza kiakili katika maisha yake ya kila siku hato shindwa kuwa kiongozi mfano kuwa mbunge.Tunatakiwa kuamsha roho ya utaifa kwa masikini na matajiri wa nchi hii wote kwa usawa na sio ombi bali liwe jukumu letu sote.Masikini ana haki pia ya kuota ndoto ya kuwa mbunge,waziri na hata rais wa nchi hii na akiishi ndoto yake,namnukuu mwanasiasa mkongwe mweusi wa Marekani bwana Jesse Louis Jackson alisema "no one should negotiate their dreams.Dreams must be free to fly high.No government.no legislature,has a right to limit your dreams.You should never agree to surrender your dreams".Kwa tafsiri hisiyo sahihi tunaweza kusema hakuna anayeweza kupanga ndoto zao,ndoto inapaswa kuwa huru na inayorendeka ,hakuna dora,hakuna bunge,lenye mamlaka ya kuweka ukomo wa ndoto zako,hupaswi kukubari kuacha ndoto zako bure.
Wito huo wa roho ya utaifa imeshatolewa,sasa au milele,maadili ya tabia njema,kufikiria hasa katika ukweli na kuwajibika na mapambano ya katiba mpya ni vitu vinavyo hitajika kwa umakini mkubwa.Songa mbele huku ukimuamini MUNGU ,na malipo yake yatajazwa mwisho wa safari....

Mwandishi na; Michael Joseph Mwanjasi